Wagonjwa wawili wameondolewa
bughdha ya kutumia madawa ya kupunguza makali ya ukimwi maishani mwao
baada ya kufanyiwa upasuaji na kupandikiziwa uboho wan binadamu au (Bone
marrow), hatua inayosemekana kuondoa virusi vya HIV mwilini mwao.
Mgonjwa mmoja amesemekana kukaa kwa miezi minne
bila ya kutumia madawa ya kupunguza makali ya ukimwi bila ya dalili ya kurejea kwa uogonjwa huo.
Madaktai waliofanya utafiti huo
katika hospitali ya matibabu kwa wanawake ya Brigham nchini Marekani,
wanasema ni mapema mno kuzungumzia uwezekano wa kutibu virusi hivyo
kwani kuna unawezekano vinaweza kurejea wakati wowote.
Matokeo ya utafiti huo yaliwasilishwa katika mkutano wa kimataifa kuhusu maswala ya Ukimwi.
Ni vigumu sana kutibu Ukimwi, kwa sababu
hujificha ndani ya DNA,ya mtu na hivyo kusababisha virusi sugu ambavyo
haviwezi kutibika.
Madawa ya kupunguza makali ya virusi vya HIV
hudhibiti virusi hivyo ndani ya damu lakini wakati mtu anapokosa kumeza dawa hizo, virusi hurejea.