Mratibu
wa Tamasha la Usiku wa Matumaini 2013, Abdallah Mrisho 'Abby Cool'
(katikati), akiongea na wanahabari leo kuhusu burudani zitakazokuwepo
siku hiyo.
Mbunge
wa Nzega, Dk Hamis Kigwangala (katikati), akielezea jinsi timu yake ya
Simba (wabunge) watakavyoigaragaza Yanga katika mechi yao.
Mbunge wa Igalula, Dkt. Athumani R. Mfutakamba (wa kwanza kushoto), akiwawakilisha wabunge wa Yanga katika mkutano huo.
Afisa
Masoko kutoka kampuni ya simu za mkononi Tigo ambao ni mmoja wa
wadhamini wa Tamasha hilo, Alex Msigala akiongea na wanahabari jinsi
kampuni yake ilivyojipanga kufanikisha Usiku wa Matumaini 2013.
Meneja Uhamasishaji Rasilimali kutoka TEA, Doreen Shekibula (katikati), akipongeza waandaaji wa Tamasha hilo.
Mwakilishi wa Bongo Fleva, H-Baba akielezea jinsi timu yake itakavyotoa kichapo kwa wapinzani wao wa Bongo Muvi.
Jacqueline Wolper (katikati) akimtumia salamu Mhe. Halima Mdee kuhusu kichapo atakachomshushia siku hiyo.
Bondia Francis Miyeyusho akiwaeleza wanahabari alivyo tayari kumkabili bondia Shadrack Muchanje kutoka Kenya.
Meneja
wa Msondo Ngoma, Said Kibiriti akiongea na wanahabari (hawapo pichani)
jinsi bendi yake itakavyowafunika wapinzani wao Sikinde.
Kiongozi wa Bendi ya Sikinde, Habib Abbas 'Jeffa' naye akielezea jinsi bendi yake itakavyofanya makamuzi siku hiyo.
---
Baadhi ya wasanii,
wabunge na wanamasumbwi watakaoshiriki katika Tamasha la Usiku wa
Matumaini 2013, leo walikusanyika katika mkutano wao na wanahabari
uliofanyika katika Hoteli ya The Atriums iliyopo Sinza jijini Dar na
kuelezea jinsi walivyojipanga kuelekea katika tamasha hilo kubwa ambalo
litafanyika Julai 7, mwaka huu katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es
Salaam. Katika tamasha hilo, wabunge wa Simba na wale wa Yanga watashuka
dimbani kucheza soka huku baadhi yao wakishiriki katika mapambano ya
ndondi dhidi ya waigizaji. Kwenye eneo la ndondi, Mhe. Halima Mdee
atapigana na Jacqueline Wolper, Mhe. Zitto Kabwe na Vincent Kigosi
‘Ray’, Mhe. Ester Bulaya atavaana na Aunt Ezekiel huku balaa zaidi
likitarajia kuandikwa na mabondia Patrick Amote (Mkenya) atakayevaana na
Thomas Mashali (Mtanzania) huku Mkenya Shadrack Muchanje akipigana na
Francis Miyeyusho (Mtanzania). Burudani nyingine zitakazokuwepo siku
hiyo ni wakali wa muziki, Nasibu Abdul ‘Diamond’ na Prezzo, ambao
watashindana katika jukwaa moja ili kutafuta nani mkali zaidi. Bendi za
Msondo Ngoma, Mlimani Park ‘Sikinde’ na Jahazi zitawaburudisha mashabiki
wao. Vilevile, burudani nyingine itatoka kwa wakali wa Temeke, Wanaume
Family na Halisi, wataokata mapanga Taifa kwa staili zao za kuvutia.
Soka la kukata na shoka kati ya Bongo Movie na Bongo Fleva litahakikisha
linawapa raha mashabiki wa wasanii watakaoingia uwanjani siku hiyo
(PICHA ZOTE : RICHARD BUKOS NA DENIS MTIMA / GPL)