Toka huu msiba umetokea kumekua na habari ambazo zinaandikwa au
kuripotiwa lakini hazina usahihi, pia habari ya kusafirishwa kwa mwili
imeandikwa tofautitofauti kwenye vyombo mbalimbali lakini uhakika ni
kwamba mwili wa Marehemu umepelekwa Airport ya Johannesburg June 3 2013
ambapo utasafirishwa june 4 kuelekea Dar es salaam na kufika mchana saa
nane.
Hizi picha zimepigwa makusudi ili kutoa ushahidi kwa wale ambao bado
walikua hawaamini kama mwili huu umefikia kwenye hatua za kusafirishwa
kutokana na kuahirishwa kusafirishwa mara mbili kwa sababu ya taratibu
za Serikali ya Afrika Kusini ambazo ilikua ni lazima zifatwe hasa
ikizingatiwa kwamba Marehemu ni kutoka nje ya nchi hii na kifo chake ni
cha ghafla.
|