Mshambuliaji wa zamani wa Prisons ya Mbeya, Yona
Ndabila ni kati ya washambuliaji waliomaliza msimu wa Ligi Kuu Nepal kwa
kuonyesha makali ya upachikaji mabao.
Ndabila ambaye aliwahi kuichezea Taifa Stars ikiwa
chini ya Marcio Maximo, alifanikiwa kupachina mabao 16 na kushika nafasi ya
pili kwa ufungaji.
Nafasi ya kwanza ilikwenda kwa mshambuliaji wa Three
Stars ambao ndiyo waliibuka mabingwa huku timu ya Ndabila, Saraswat Youth Club
ikishika nafasi ya tisa na kukosa nafasi ya kucheza nane bora.
Akizungumza na Salehjembe, Ndabila amesema
anatarajia kurejea nchini humo Juni kujiandaa na ligi ambayo itaanza Julai.
“Niko nyumbani Mbeya nimekuja kuwaona wazazi, mwezi
wa sita nitarejea kazini maana ligi inaanza mwezi wa saba,” alisema Ndabila.
Ndabila ambaye alionyesha kukata tamaa soka ya
Tanzania, amekuwa mmoja wa wachezaji maarufu wa ligi hiyo.
Klabu yake imekuwa ikikataa kumuachia kutokana na
kumuona ni tegemeo katika upachikaji wa mabao.
Kiana, hivi karibuni Ndabila alimvuta kiungo wa
zamani wa Prisons, Yanga na Mbeya City, Godfrey Bonny ‘Ndanje’ ambaye pia
ameanza kuonyesha makali yake.