Jose
Mourinho amesema Real Madrid inaweza kuwafunga Dortmund licha ya Robert
Lewandowski (chini) kuwapa wastani wa mabao matatu yanayotakiwa
kufungwa na Madrid ili kusonga mbele.Wakati
huo huo kocha wa Borussia Dortmund Jurgen Klopp alisistiza kuwa timu
yake haitapaniki hata kidogo kupamBana na Real Madrid katika uwanja wao
kwani wanajua watakuwa wanahitaji ushindi kwa nguvu zote.
Flopp aliongeza kuwa ushindi wa 4-1 nyumbani ni mkubwa sana na hadhani kama watakubali kuupoteza leo hii mbele ya Mourinho.
Alipoulizwa kama kama timu yake itashinda mchezo wa leo Flopp alisema “No, sina uhakika lakini nadhani hatuwezi”.
Huyu bwana hakufanyiwa hata rafu moja ndani ya dakika 90 licha ya kufunga mabao manne pekee yake
Wachezaji wa Real Madrid wakifanya mazoezi kabla ya mchezo wao wa usiku dhidi ya Dortmund uwanja wa Santiago Bernabeu
Sergio Ramos (kushoto) na Xabi Alonso wakipasha misuli yao leo kabla ya mchezo wao wa usiku
Flopp
ana uhakika na alisema “Tulicheza na Bayern fainali ya kombe la
Ujerumani wakati tayari tukiwa mabingwa. Walihitaji sana ushindi
kufuatia kuwa na msimu mbaya, lakini timu yangu ilitulia na kuwapoteza
kwa wastani wa maboa 5-2.“Nadhani hata Madrid wataingia na falsafa hii
ili kututoa, lakini kama hawa amini hivyo najua watambana sana”. Alisema
Flopp.
Klopp na Ilkay Gundogen wakiwa katika mkutano kabla ya mechi dimbani Bernabeu.
Maandalizi: Dortmund wakifanya mazoezi kabla ya mchezo wao wa leo usiku
Lewandowski
(kushoto) ambaye aliwafunga Madrid 4 na mechi iliyopita dhidi ya
Fortuna Dusseldorf ligi kuu soka nchini Ujerumani “Bundesliga”
alipumzishwa kwa ajili ya kipute cha leo.
Wakipasha: Marco Reus (kushoto) na Mario Gotze (kulia) wakipiga jalamba
Na Baraka Mpenja kwa Msaada wa Sportsmail.com
Kocha
wa Real Madrid Mreno Mario Jose Dos Santos Ferlix Mourinho bado ana
imani kubwa kuwa kikosi chake kitabadili kipigo cha mabao 4-1
walichokipata huko Ujerumani katika mchezo wao wa marudiano dimbani
Santiago Bernabeu.
“Timu yangu mara siku zote inafanya vitu vya haki, na inaweza kushinda kwa haki katika mchezo wa leo”. Alisema Mourinho leo hii.
Kocha
huyo aliendelea kusema “Tumekubali kuwa Lewandowski alitufunga mabao
manne na hatukumfanyia hata faulo mojo. Lakini Dortmund walimfanyia
Ronaldo madhambi mara tano tangu mchezo kuanza”.
“Unawezaje
kumaliza dakika 90 bila kumfanyia madhambi mchezaji aliyekufunga mabao
manne pekee yake, ndio maana nasema timu yangu inacheza kwa haki”.
Alisisitiza Mourinho.
Leo
hii Madrid wanaingia uwanjani wakiwa na kibarua kizito cha kupindua
kipigo cha 4-1 kutoka kwa nyuki wa kaskazini mashariki mwa Ujerumani.
Mabao
yote ya Dortmund yalitiwa kambani na Robert Lewandowski lakini Mourinho
alisema timu yake haikumkaba vizuri na ndio maana Mpoland huyo
hakufanyia madhambi hata kidogo.