Utafiti uliofanywa mwaka 1940 ulionyesha kuwa asilimia 50 ya nguvu za
kiume hushuka kutokana na kiwango kikubwa cha unywaji wa uvutaji wa
sigara, pombe pamoja na mabadiliko ya mazingira. Pia uvutaji wa sigara 20 kwa siku na ulaji wa chipsi, baga, soseji inachangia kwa asilimia 43 kuharibu nguvu za kiume. |
HALI ya maisha pamoja na mazingira husika yanayomzunguka binadamu imeelezwa kuwa ni chanzo cha kushuka kwa nguvu za kiume.
Madaktari wengi wameripoti juu ya kuwepo kwa
ongezeko la wagonjwa wengi wa kiume ambao wamekuwa wakilalamikia juu ya
upungufu wa nguvu za kiume.
Mwaka jana mwishoni gazeti la The Independent llilopo nchini Uingereza liliripoti kuwa hali ya afya ya viungo vya uzazi hususani kwa wanaume ilishuka kwa kiwango kikubwa na hiyo ilitokana na utafiti uliofanywa duniani juu ya ubora wa mbegu za kiume.

Utafiti huo ulionyesha kuwa katika miaka ya 1989
hadi 2005 ulionyesha kuwa kati ya wanaume 26,000 waliofanyiwa uchunguzi
robo tatu yake walionekana kuwa na uwezekano mkubwa wa kushindwa kuzaa.
Mwaka 1989 na 2005, kwa mujibu wa gazeti moja la
Uingereza lilisema kwamba “Wanaume 26,000 wanakabiliwa na tatizo hilo
la upungufu wa mbegu za kiume.’’
Utafiti huo uliendelea kufanyika ili kuhakikisha juu ya uchunguzi uliofanyika miaka 20 iliyopita na matokeo yake yalizidi kuonyesha kuwa nguvu za kiume zimezidi kudhoofika kwa wanaume wengi duniani.
Utafiti huo uliendelea kufanyika ili kuhakikisha juu ya uchunguzi uliofanyika miaka 20 iliyopita na matokeo yake yalizidi kuonyesha kuwa nguvu za kiume zimezidi kudhoofika kwa wanaume wengi duniani.
Miongoni mwa sababu ambazo zimekuwa zikisababisha
nguvu hizo kuporomoka ni pamoja na kuvaaji wa nguo za ndani ambazo
zinabana, pia wataalamu walieleza kuwa ufumbuzi juu ya sababu maalumu
ya nguvu hizo kushuka bado haujapatikana.
Baadhi ya waandishi nchini Kenya hususan katika gazeti la Daily Nation waliamua kufanya utafiti juu ya hilo ili kuweza kufahamu kama tatizo hilo lipo nchini humo.
Baadhi ya waandishi nchini Kenya hususan katika gazeti la Daily Nation waliamua kufanya utafiti juu ya hilo ili kuweza kufahamu kama tatizo hilo lipo nchini humo.
Utafiti huo ulifanywa na daktari mmoja maarufu
katika Hospitali ya Royal Garden nchini humo aliyejulikana kwa jina la
Solomon Wasike ambaye alisema kuwa wiki mbili zilizopita alipata mgonjwa
mwenye tatizo kama hilo.
Aliongeza kuwa mwanamume huyo alikuwa na umri wa
mika 28 alikuwa amefika katika kliniki yake kwa ajili ya kupima juu ya
uwezo wake wa kuzaa.
Hali hiyo ilikuja baada ya kufunga ndoa na mke wake mwaka mmoja uliopita lakini hadi sasa mwanamke huyo alishindwa kupata mimba.
Hali hiyo ilikuja baada ya kufunga ndoa na mke wake mwaka mmoja uliopita lakini hadi sasa mwanamke huyo alishindwa kupata mimba.
Daktari Wasike alisema kuwa baada ya maelezo hayo
aliamua kuchukua mbegu zake mwanaume huyo kwa ajili ya vipimo
aliongeza kuwa majibu yake yalikuwa na utata kwa kuwa yalionyesha kuwa
mtu huyo alikuwa na uwezo mdogo wa kuzalisha mbegu hali ambayo
iliyosababisha mke wake kutopata mimba.
Wasike alisema kuwa hali hiyo imekuwa ikijitokeza
mara kwa mara katika kliniki hiyo kuwa na wagonjwa wengi wa kiume wenye
matatizo katika afya ya uzazi.
“Kinachotusumbua ni kwamba vijana wengi wanaokuja
katika hospitali hii wamekuwa na matatizo sawa katika mbegu za kiume na
jambo hili linazidi kusikitisha kwa kuwa asilimia kubwa ya watu
wanaokuja ni vijana.
Aliongeza kuwa hali hiyo inafanya tuamini kuwa
licha ya wengine kuwa na matatizo hayo tangu kuzaliwa lakini asilimia
kubwa ya vijana wanapatwa na tatizo hilo kwa sababu ya hali ya maisha
wanayopitia pamoja na mazingira wanayoishi.
Hata hivyo takwimu za kitaifa bado hazijafanywa
juu ya tatizo licha ya kuwa kumekuwa na malalamiko mengi ya wanaume
kutoka katika katika hospitali mbalimbali.
source:MWANANCHI
source:MWANANCHI