BINGWA WA AFCON 2013 KUPATIKANA JUMAPILI HII KATI YAN NIGERIA NA BURKINAFASO

AFCON 2013: BINGWA KUPATIKANA JUMAPILI KATI YA NIGERIA NA BURKINA FASO, MSHINDI WA TATU KESHO JUMAOSI.

Nigeria

Burkina Faso
Mbabe wa Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2013, atajulikana Jumapili baada ya miamba ya soka barani Afrika, Nigeria na Burkina Faso kupambana katika mchezo wa fainali.
Fainali za mwaka huu zinazofanyika nchini Afrika Kusini, zilishirikisha timu 16, huku mabingwa watetezi wa kombe hilo, Zambia, waking'olewa katika hatua ya makundi.
Timu nane zilisonga hatua ya robo fainali.

Timu hizo ni Afrika Kusini, Burkina Faso, Cape Verde, Ghana, Ivory Coast, Mali, Nigeria na Togo.
Nigeria ambayo ilianza kwa kusuasua katika hatua ya makundi, imeonyesha mchezo mzuri katika mechi zake zilizofuata kuanzia ngazi ya robo na nusu fainali.

Ikicheza hatua ya robo fainali, Nigeria iliifunga Ivory Coast mabao 2-1, huku Ghana ikiifunga Cape Verde mabao 2-0.

Baada ya kutinga nusu fainali, Nigeria iliiadhibu Mali magoli 4-1. Nayo Burkina Faso ikishinda magoli 3-2 kwa mikwaju ya penalti baada ya sare ya 1-1 dakika 120 za mchezo.

Mali sasa itapambana na Burkina Faso kutafuta mshindi wa tatu siku ya Jumamosi.
Party atmosphere: Nigerian fans celebrate their progress
Iwe isiwe, bingwa ni kati ya Nigeria na Ghana

REFA ALIYECHEZESHA MECHI YA AFCON KATI YA BURKINA FASO NA GHANA AFUNGIWA !


Kipa wa Ghana, Fatau Dauda (kulia) na Kwadwo Asamoah wakilinda goli lao huku Prejuce Nakoulma wa Burkina Faso akijaribu kufunga wakati wa mechi yao ya nusu fainali ya Mataifa ya Afrika kwenye Uwanja wa Mbombela mjini Nelspruit jana Februari 6, 2013. Picha: REUTERS

Wachezaji wa Ghana wakiwa hoi baada ya kupoteza mechi yao ya nusu fainali ya Mataifa ya Afrika dhidi ya Burkina Faso kwenye Uwanja wa Mbombela mjini Nelspruit jana Februari 6, 2013. Burkinabe walishinda kwa penalti 3-2 baada ya sare ya 1-1. Picha: REUTERS

Wachezaji wa Ghana wakiwa hoi baada ya kupoteza mechi yao ya nusu fainali ya Mataifa ya Afrika dhidi ya Burkina Faso kwenye Uwanja wa Mbombela mjini Nelspruit jana Februari 6, 2013. Picha: REUTERS

REFA Mtunisia Slim Jdidi amefungiwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kufuatia maamuzi ya utata katika mechi ya nusu fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika juzi baina ya Burkina Faso na Ghana.

"CAF haijafurahishwa na kiwango cha uamuzi katika mechi ile," katibu mkuu Hicham El Amrani aliviambia vyombo vya habari.

"Tunajua kwamba wanaweza kufanya makosa lakini tunatarajia kiwango kizuri zaidi cha uamuzi. Wanawekewa viwango kulingana na kila mechi waliyochezesha na kulingana na maksi zake, refa kutoka Tunisia sasa amefungiwa kwa muda ambao bado haujaamuliwa."
 
© 2012. Design by Ernest James Siwigo Chambasi - Supported By John James Chambasi And Maganza Family