Wanafunzi
wa Chuo Cha Uongozi wa Fedha cha jijini Dar es Salaam (IFM) wakiwa
mbele ya geti la Wizara ya Mambo ya ndani walipovamia leo majira ya saa
nne nanusu asubuhi wakiwa na madai ya kutopewa ulinzi na jeshi la
polisi kwenye makazi yao ya Hosteli za Kigamboni kutokana na kuvamiwa
na majambazi mara kwa mara. Wanafunzi hao walidai siku ya Ijumaa
walifanya kikao na jeshi hilo ili wawape ulinzi lakini suala la ajabu
siku waliyofanya kikao na Jeshi hilo ndio siku waliovamiwa wenzao
wawili wakiume na kubakwa hali iliyosababishwa wanafunzi hao kubakwa.
Majambazi hao wamekua wakidai kupewa Laptop simu na fedha kama
mwanafunzi akikataa humfanyia vitendo vya kulawiti.
|