WAZIRI wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Kimataifa,
Bernard Membe
----
WAZIRI wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Kimataifa,
Bernard Membe ametangaza kuwa hatogomea tena ubunge katika uchaguzi mkuu
ujao.
Membe ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Mtama, mkoani Lindi,
alitoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza kwenye sherehe za Mwaka Mpya nyumbani
kwake.
“Unajua nimekuwa mbunge wenu kwa kipindi cha tatu. Hivi
leo ninawaaga rasmi kuwa sitagombea tena nafsi hii ya ubunge,” alisema
Membe.
Ambapo pia
aliwataka wananchi wa mikoa ya kusini, kuwa na subira katika kipindi hiki ambapo
Serikali inashughulikia mchakato wa kuvuna gesi asilia.Alisema kuwa ni muhimu
kwa wakazi wa mikoa iliyopatikana gesi kutambua kuwa rasilimali zilinazopatikana
nchini ni mali ya Watanzania wote na siyo ya mikoa iliyogundulika
pekee.
Waziri Membe aliwataka madiwani wa Halmashauri ya
Wilaya ya Lindi, kuacha kutumia vikao vya halmashauri kujadili malumbano
yasiyokuwa na msingi akisema kwamba kufanya hivyo ni kipoteza rasilimali za
wananchi bila faida.