MSANII nyota wa miondoko ya Mnanda a.k.a Mchiriku, Omari Omar amefariki
dunia usiku wa kuamkia leo baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Habari zilizoifikia MICHARAZO, asubuhii zinasema kuwa, Omar Omar
aliyetamba na nyimbo mbalimbali ukiwemo ule maarufu wa 'Kupata ni
Majaliwa' alifariki nyumbani kwao Temeke, saa chache baada ya kurejeshwa
toka hospitali ya temeke alipokuwa amelazwa kwa siku kadhaa.
Taarifa hizo zinasema kuwa mara baada ya kurejea nyumbani, msanii huyo
alizidiwa na hatimaye kufariki na kwamba msiba wake upo nyumbani kwao
Temeke Mikoroshini kwa ajili ya mipango ya mazishi.
Msiba wa msanii huo umekuja siku chache baada ya tasnia ya sanaa na
burudani kumpoteza Juma Kilowoko 'Sajuki' msanii nyota wa filamu
aliyefariki pia kutokana na kusumbuliwa na maradhi ya muda mrefu.
MICHARAZO inawamuombea kila la heri Omar Omar na wengine waliotangulia
mbele ya haki mapumziko mema katika safari yao ya Ahera. Innallillah
Waina Illah Rajiun.
Taarifa zaidi tutakuwa tunawaletea kujua mkali huyo wa mduara
aliyewafanya wasanii wengine kufuata mkondo wake akiwemo Dogo Mfaume,
Ferouz, Easy Man na wengine.