RAIS KIKWETE ATANGAZA MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI ILIYOFANYIKA MWAKA 201

Hii ndiyo idadi ambayo imetangazwa na Rais Jakaya Kikwete leo kwenye uzinduzi matokeo ya Sensa iliyofanyika nchini kote mapema mwaka huu (2012)
 Rais Jakaya Kikwete, akizungumza na wananchi wakati akisoma hotuba yake ya kutangaza rasmi uzinduzi wa matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi, leo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Rais Jakaya, alisema kuwa katika Sensa ya mwaka huu, watanzania wameongezeka kwa asilimia kubwa ukilinganisha na Sensa iliyofanyika kwa mara ya kwanza nchini ya mwaka 1967, ambapo Watanzania wote walikuwa ni Milioni 12, 313, 054, na Tanzania Bara walikuwa ni milioni 11, 958,654 na Visiwani Zanzibar, walikuwa ni 354, 400, ambapo baada ya mwaka huo, Sensa kama hiyo ilifanyika tena mwaka 1978, 1988,2002 na hii ya mwaka huu 2012, ambapo imetoa idadi ya Watanzania wote kuwa ni jumla ya Milioni 44, 929,002. 
  
 Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa wa Shirika la Idadi ya Watu Duniani akihutubia wakati wa hafla hiyo
 Kamishina wa Sensa,  akipongezwa na  viongozi wa serikali kwa kufanikisha sensa hiyo
 Baadhi ya Madiwani na viongozi mbalimbali wa Serikali, waliohudhuria katika hafla hiyo leo.
 Baadhi ya wakazi wa Dar es Salaam wakishangilia huku wakiwa na mabango  ya kumpongeza Rais Jakaya Kikwete
 Kikundi cha Uhamasishaji cha Temeke, akikiwa ni miongoni mwa wageni waalikwa kilichokuwa kikiendelea na kazi yake ya uhamasishaji uwanjani hapo.
 Sehemu ya wananchi waliojitokeza kuhudhuria hafla hiyo.
 Bendi ya THT, kutoka (kulia) ni Marlow, Amin na Linah, wakitoa burudani jukwaani wakati wa hafla hiyo.
 Wananchi wakisebeneka kushangilia baada ya Rais Jakaya Kikwete, kutangaza rasmi matokeo hayo ya Sensa.
 Picha ya pamoja kwa kumbukumbu.
 Picha ya pamoja kwa kumbukumbu.
 Picha ya pamoja kwa kumbukumbu.
  
Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba akimpongeza Rais Kikwete kwa kufanikisha sensa hiyo
Rais Jakaya Kikwete, akiteta jambo na Mwenyekiti wa CUF, Ibrahim Lipumba, wakati akiondoka katika viwanja vya Mnazi Mmoja, baada ya kuzidua rasmi matokeo ya Sensa ya watu na makazi
 Rais Jakaya Kikwete (kulia), Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (katikati) na  Mwenyekiti wa Kampuni za IPP, Reginald Mengi wakicheka kwa furaha baada ya uzinduzi huo.
 
© 2012. Design by Ernest James Siwigo Chambasi - Supported By John James Chambasi And Maganza Family