Barnaba amedai kuwa msanii wa DRC, Fally Ipupa ni mtu anayefurahia kipaji chake.Kwa miaka mingi Barnaba amekuwa na mpango wa kumshirikisha msanii huyo. Hata hivyo ameiambia Bongo5 kuwa anachoshukuru ni kwamba bado wanazungumza vizuri ili kuweka mpango huo wa kufanya kazi pamoja. “Kwanza ni mtu anayenifurahia,” amesema Barnaba. “Fally anafurahia kipaji changu, anapenda talent niliyonayo, halafu ni mtu ninayempenda, ni role model wangu. Pia anafurahia uwepo wangu kwa sababu ni nembo yake. Nafanya kazi kupitia mgongo wake, tunaongea vizuri kwa sababu tunatumia lingala na tunavyo chati tunachati lingala, ingawa kuna muda napata shida kwa sababu anaongea French ila kila kitu kipo sawa.” |
TRA Iringa yawashukuru walipa kodi wake
6 hours ago