Waziri wa Nishati na
Madini Mhe. George Simbachawene (kushoto)
akizungumza na waandishi wa habari mara
baada ya kupokelewa na uongozi wa Wizara
hiyo. Kulia ni Kaimu Katibu Mkuu
wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi
Ngosi Mwihava. Mhe. Simbachawene amesisitiza umuhimu wa sekta za nishati na
madini kama mhimili mkuu wa ukuaji wa uchumi wa nchi na kuomba
ushirikiano kutoka kwa wadau mbalimbali wa sekta za nishati na madini.
Waziri wa Nishati na
Madini Mhe. George Simbachawene
(kushoto) akipokea ua la maua kutoka
kwa mmoja wa watumishi wa Wizara ya
Nishati na Madini Lilian Aroko mara
baada ya kuwasili kwenye ofisi za Makao Makuu ya Wizara ya Nishati na Madini.
Naibu Waziri wa Nishati na
Madini (Nishati) Mhe. Charles Mwijage
(Kulia) akimpokea Waziri wa Nishati na
Madini Mhe. George Simbachawene
(kushoto) mara waziri huyo alipowasili kwenye Ofisi za Makao Makuu ya
Wizara ya Nishati na Madini.
Waziri wa Nishati na
Madini Mhe. George Simbachawene (kulia)
akisalimiana na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya
Sheria, Salome Makange mara baada
ya kuwasili kwenye Ofisi za Makao Mkuu ya Wizara.