Kituo cha ITV kimeripoti kuwa Jeshi la Polisi limetumia mabomu ya machozi kuwatawanya wafuasi wa Chama cha Wananchi CUF, waliokuwa wanaenda kushiriki katika mkutano wa kuwa kumbuka wanachama wenzao waliouwawa huko Zanzibar mwaka 2001, na kutumia nguvu kubwa kuwatawanya Waandishi wa Habari, ambapo Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho Pro. Ibrahim Lipumba na viongozi wengine walipigwa na kuwekwa chini ya ulinzi wa Polisi.
Hali hiyo ilianza katika Ofisi za CUF Temeke baaada ya Pro. Lipumba kuwatangazia wafuasi hao kuwa, hakutakuwa na maandamano ya kwenda katika viwanja vya Mbagala Zakem na badala yake atakwenda mwenyewe kuwatangazia wananchi ambao tayari walikuwa wameanza kukusanyika katika eneo hilo la mkutano.
“Wameiweka kwa makusudi kwasababu
wanahitaji kuuwa watu wanahitaji watu wanajua kabisa kwamba kuna
maandamano, Polisi wamezuia maandamano wanatupa taarifa wakati viongozi
hawawezi kuipata taarifa hiyo, hakuna muda wa kuweza kuwasiliana na
wananchi, kwa hiyo hili ni jambo lililofanywa kwa makusudi wala sio kwa
bahati mbaya, kwa hiyo nawaomba nyie muweze kutulia kuweza kurudi kwenye
shughuli zenu mimi nakwenda viwanja vya zakim kwasababu watu hawana
taarifa watu wamekwenda kwenye viwanja vya mkutano hawana taarifa kama
maandamano haya na mkutano wao umezuiliwa”–Alisema Pro. Lipumba
Hata hivyo Jeshi la Polisi lilifanikiwa kuyadhibiti maandamano hayo yaliyoleta tafrani kubwa kwa wananchi wa eneo hilo.