UNAJUA KUHUSU UKIMYA WA PRODUCER LAMAR?BASI USOME HAPA

Lamar
Mtayarishaji wa muziki Lamar, ameweka wazi kuwa hajaishiwa ubunifu katika utayarishaji wa muziki lakini amefanya kazi nyingi za wasanii ambao hawataki kuziachia hali inayochangia aonekane kuwa kimya.

Kazi zake pekee zinazosikika hivi karibuni ni zile za kurudia nyimbo na kuzitengeneza katika mahadhi ya house, Refix.

“Siku zote mimi niko tofauti, ujue watu hawaelewi mimi narekodi nyimbo
lakini sina mamlaka ya ku-release wimbo wa msanii mpaka artist mwenyeweakubali ndio maana naonekana nipo kimya,” amesema Lamar.

“Lakini tracks narekodi kama kawaida na zipo bado kwenye library mpaka
msanii mwenyewe awe tayari kuirelease ndio naziachia na utazisikia katika redio ndio hapo utajua kuwa mimi nimefanya kazi.”
 
© 2012. Design by Ernest James Siwigo Chambasi - Supported By John James Chambasi And Maganza Family