Jux na Vanessa Mdee hawataki tena kuficha uhusiano wao. Tangu mwaka mpya uanze, waimbaji hao wameuachia ulimwengu ufahamu kuwa ni wapenzi na wanapendana baada ya kipindi kirefu cha tetesi za uhusiano wao ambazo walikuwa wakizikanusha.Uhusiano huo umepelekea hadi Jux amtumie Vee Money kama mpenzi wake kwenye video ya ‘Sisikii’ na kama umeitazama utakuwa umegundua chemistry ya kuvutia kati yao. Weekend hii wawili hao wakiwa pamoja na Navy Kenzo, walikuwa na show visiwani Zanzibar ambapo Jux pamoja na kutumbuiza nyimbo zake, alipanda jukwaani kumpa kampani mpenzi wake huyo kwa kuchukua nafasi ya Barnaba wakati alipokuwa akitumbuiza wimbo ‘Siri’. Baada ya show hiyo wapenzi hao walijumuika pamoja kula upepo kwenye beach za Zanzibar na mashabiki wao wanafurahia tu kuwaona pamoja. |