Kundi la Navy Kenzo na Shaa wameungana na Diamond Platnumz kwenye chart za Africa Rox Countdown zinazorushwa na kituo maarufu cha runinga cha Sound City cha nchini Nigeria.Hiyo ina maanisha kuwa Tanzania ni nchi pekee yenye wasanii wengi katika chart hizo. Navy Kenzo wameingia kwenye chart hiyo inayozikutanisha nyimbo 10 zinazofanya vizuri zaidi barani Africa na video ya wimbo wao ‘Moyoni’ wakishika nafasi ya tisa. Naye Shaa amekamata nafasi ya 10 na video ya wimbo wake ‘Njoo’ aliomshirikisha Redsan, huku Diamond aliyetangulia kuwepo kwenye chart hizo akikamata nafasi ya 7 na wimbo wake ‘Ntampata Wapi’. Wasanii wengi wa Afrika waliomo kwenye chart hiyo ni pamoja na D’Banj, Emmy G, Eddy Kenzo wa Uganda, Sarkodie, AKA na Casper Nyovest. Kipindi hicho kinaendeshwa na VJ Adams. |