Kundi la Weusi limemeingia tena studio, lakini safari hii
wakiwa na rapper Navio kutoka Uganda ambaye yupo jijini Dar es salaam
kwa sasa. Weusi wamemuongeza Navio kwenye remix ya single yao ‘Gere’, ambayo tayari walitangaza kuwa wameifanyia remix nchini Kenya miezi kadhaa iliyopita na kuwashirikisha Collo na Naziz na hivyo kuifanya kuwa ni remix iliyohusisha wasanii wa nchi tatu za Africa mashariki, Tanzania, Kenya na Uganda. Joh alishare picha Instagram akiwa studio na Navio, Nahreel, Lordize na G-Nako na kuandika: /“Studioni saa hii with @naviomusic @gnakowarawara @nahreel #Lordize #Gere Eastafrican remix feat.#collo #naziz”/ aliandika Joh Makini Instagram. |