Mgeni rasmi katika Tamasha la Usiku wa Matumaini 2014, Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Ghalib Bilal akitoa hotuba.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Global Publishers Ltd ambao ndiyo waandaaji wa Tamasha la
Usiku wa Matumaini 2014, Eric Shigongo naye akitoa neno la matumaini kwa
maelfu ya Watanzania waliofurika Uwanja wa Taifa, Dar.
Dk. Mohammed Gharib Bilal akiongea jambo na refa wa mchezo wa mechi ya wabunge akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Global, Eric Shigongo.
Makamu
wa Rais wa Tanzania, Mohamed Ghalib Bilal amelipongeza wazo la Tamasha
la Usiku wa Matumaini lililoandaliwa na Kampuni ya Global Publishers,
jana kuwa ni zuri.
Alimpongeza Mkurugenzi wa Global Publishers, Eric Shigongo kwa kuandaa tamasha hilo kwani linaunganisha Watanzania wote.