Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete (katikati) na balozi mdogo wa Japan nchini
Kazuyoshi Matsunaga (wa tatu kushoto) wakishirikiana kukata utepe ikiwa
ni ishara ya kuzindua ujenzi wa Barabara ya Tunduru-Mangaka Matemanga
mradi unaojengwa na Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano wa serikali ya
Japan kupitia shirika lake la kimataifa la maendeleo JICA.Wengine
pichani toka kushoto ni ni Mbunge wa Nanyumbu Dunstan Mkapa,Mkuu wa Mkoa
wa Mtwara,Kapten Mstaafu Joseph Simbakalia,Waziri wa ujenzi Dkt. John
Pombe Magufuli, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete,Wairi wa Ardhi nyumba na
mendeleo ya makazi Profesa Anna Tibaijuka na Waziri wa TAMISEMI,Hawa
Ghasia.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza balozi mdogo wa Japan Kazuyoshi
Matsunaga muda mfupi baada ya kuzindua ujenzi wa Barabara ya
Tunduru-Mangaka Matemanga mradi unaojengwa na Serikali ya Tanzania kwa
ushirikiano wa serikali ya Japan kupitia shirika lake la kimataifa la
maendeleo JICA.Kushoto ni mbunge wa Nanyumbu Dunstan Mkapa, wapili
kushoto ni Waziri wa ujenzi Dkt.John Pombe Magufuli, Mke wa Rais Mama
Salma Kikwete na kulia ni Wairi wa Ardhi nyumba na mendeleo ya makazi
Profesa Anna Tibaijuka
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifungua maji katika kisima kuashiria
kuzindua rasmi mradi wa maji katika kata ya Nalasi wilayani
Tunduru.Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Chande Bakari
Nalicho,Wapili kulia anayepiga makofi ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said
Mwambungu na kulia ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimtwisha ndoo ya maji mkazi wa kata ya
Nalasi Rehema Kassim Yakubu wakati alipokwenda kuzindua mradi wa maji
katika kata hiyo iliyopo katika wilaya Tunduru leo.(picha na Freddy
Maro)