Mwimbaji wa Nyimbo za Injili Bahati Bukuku akiwa kwenye moja ya kazi zake ya uimbaji.
Na: Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Dodoma.
Gari
lenye namba IT 7945 aina ya Toyota Nadia ikiendeshwa na EDSON S/O
MWAKABUNGU, Mnyakyusa, Miaka 31 mkazi wa Tabata – Dar es Salaam liliacha
njia na kugonga gema na kusababisha majeruhi kwa watu watatu baada ya
kugongwa na gari lingine linalosadikiwa kuwa ni Fuso.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID
MISIME – SACP amesema ajali hiyo imetokea tarehe 26.07.2014 majira ya
saa 03:00 alfajiri katika barabara kuu ya Morogoro – Dodoma eneo la
Ranch ya NARCO Wilaya ya Kongwa.
Kamanda
MISIME amewataja waliojeruhiwa katika ajali hiyo kuwa ni EDSON s/o
MWAKABUNGU ambaye analalamika maumivu sehemu za vidole vya miguu yote,
BAHATI D/O BUKUKU, Miaka 40, Mnyakyusa, Msanii wa nyimbo za Injili na
mkazi wa Tabata – Dar es Salaam ambaye analalamika maumivu sehemu
mbalimbali za mwili wake na FRANK S/O CHRISTOPHER, Muha, Miaka 20,
Msanii wa muziki wa Injili mkazi wa Tabata Dar es Salaam yeye ana
michubuko usoni na mkono wa kulia. Wote wamelazwa katika Hospitali ya
Wilaya ya Kongwa kwa matibabu na hali zao zinaendelea vizuri.
Aidha
Kamanda MISIME ameongeza kwa kusema kuwa watu walikuwa wanatokea Dar es
Salaam ambapo dereva alikuwa anelekea DRC – Kongo, BAHATI d/o BUKUKU na
FRANK s/o CHRISTOPHER walikuwa wanakwenda Kahama kwenye tamasha la
Injili.
Uchunguzi wa ajali hii unaendelea ikiwa ni pamoja na kutafuta gari lililowagonga.
|