SAMATTA,KASEJA NA NGASSA WACHAGULIWA KUWANIA "TUZO ZA WATU"


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiWzwH08j2lu0If6W-Qa1sdrAD6AFFCmju-BPTsrLafqAOBR5MM1vZiqEu97TTKHAQ_8zmyYYFE1llYlxVHfipXDYKGstIF-yETR44Wjwy43P9TjuOSfMAAKkLQBYGYFTsFHtIJfXzi23E/s1600/samatta2.jpg
WACHEZAJI Mbwana Samatta wa TP Mazembe ya Jamburi ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Mrisho Ngassa na Juma Kaseja wa Yanga wanawania tuzo ya mwanamichezo bora inayojulikana kama tuzo za watu.
Mbali na wachezaji hao, wengine wanaowania tuzo katika kipengele hicho cha wanamichezo ni Ramadhani Singano wa Simba na bondia Francis Cheka. Tuzo hizo mpya zinaandaliwa na kampuni ya Bongo 5media Group na washindi watatangazwa Juni mwaka huu.
Kwa mujibu wa Mhariri Mkuu wa tovuti hiyo, Fredrick Bundala, tuzo za watu zinashindanisha wanamichezo, watangazaji, wasanii, vipindi vya redio na waongozaji video na kila kipengele kitatoa mshindi wake atakayepatikana kwa mashabiki kupiga kura.
Alisema kwa upande wa wanamichezo, wachezaji hao ndio waliopata kura nyingi na hivyo wameingia kwenye shindano.
Baadhi ya tuzo nyingine ni muigizaji wa kike wa filamu inayowaniwa na Elizabeth Michael ‘Lulu’, Jacqueline Wolper, Shamsa Ford, Irene Uwoya, Wastara Juma na kwa upande wa wanaume ni Jacob Stephen ‘JB’, King Majuto, Vincent Kigosi ‘Ray’, Hemed Suleiman ‘PHD’ Salim Ahmed ‘Gabo’.
Bundala alisema kuwa filamu ni pamoja na Foolish Age ya Lulu, Bado Natafuta ya Salim Ahmed pamoja na Shamsa Ford, Shikamoo Mzee ya JB, Shamsa Ford na King Majuto, Ndoa Yangu ya marehemu Steven Kanumba na Wolper pamoja na Zawadi Yangu ya JB na Irene Uwoya.
Kwa upande wa mtangazaji wa runinga wanaoshindanishwa ni pamoja na Salama Jabir na Sam Misago wa East Africa Television, pia yupo Zamaradi Mketema wa Clouds Tv, Salim Kikeke wa BBC Swahili na Gondwin Gondwe wa ITV.
Bundala aliwataka Watanzania kuwapigia kura wale wanaowapenda kwa kutuma ujumbe mfupi wa neno TUZO kwenda 15678 na baadaye kufuata maelekezo rahisi ya kupiga kura pia kupitia tovuti www.tuzozetu. com.


 
© 2012. Design by Ernest James Siwigo Chambasi - Supported By John James Chambasi And Maganza Family