![]() |
Ni
kawaida sasa hivi kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii na baadhi ya
blogs na website kuweka picha za uchi au mitandao ambayo imekua maalum
kwa ajili ya kueneza picha na video zikionyesha watu wakiwa uchi.
Unaambiwa Kenya sasa hivi yeyote anaetuma msg zenye matusi au
kusambaza picha za watu wakiwa uchi kwenye mitandao ya kijamii kama vile
facebook na twitter atafungwa jela kwa miezi mitatu au kulipa faini ya
zaidi ya shilingi laki tisa za Kitanzania.
Kwa mujibu wa Radio Jambo, Mamlaka ya mawasiliano Kenya imetoa ripoti
ikionyesha utumaji wa picha za watu wakiwa uchi na utazamaji wa
mitandao ya ngono ulipanda kwa asilimia 60% mwezi April 2014 nchini
Kenya.
|

