BONDIA THOMAS MASHALI APATA AJALI

Bondia Thomasi Mashali akionesha majeraha aliyoyapata baada ya kupata ajali hivi karibuni picha nawww.superdboxingcoach.blogspot.com


=====  =====  ======
BONDIA Thomasi Mashali amepata ajali ya gari mara baada ya kuangukia mtaloni akiwa anaendesha gari aina ya vitz lenye namba za usajili T 777 BMW ajari hiyo iliyotokea maeneo ya kimara baruti siku ya april 20
wakati akitokea manzese kwenda nyumbani kwake kimara mwisho, akielezea tukio zima la ajali hiyo Mashali 'Alisema nilikuwa naendesha mwenyewe nikakutana na tuta nikaruka tuta nilivyomaliza tu tuta kumbe mbele yangu kulikuwa kumefungwa kutokana na matengenezo ya barabara ya morogoro  ile nataka kukwepa uzio ambapo nilipo kwepea nika ingia mtaloni moja kwa moja
katika gari hiyo tulikuwa wawili na mdogo wangu George Maluma ambaye ajaumia chochote katika ajari hiyo
akizungumzia mchezo wake unao mkabili ambao ulikuwa ufanyike siku ya mei mosi katika ukumbi wa PTA Sabasaba kwa ajili ya kumkabili Kalama Nyilawila, mashali alisema kuwa kwa sasa sifanyi mazoezi kwa kuwa nauguza majeraha yangu ya kuchubuka na kutoka kwa ngozi katika mkono wangu wa kulia na ubavuni mwangu
namwambia Kalama kuwa kafala laker limegonga mwamba hivyo akae tayali kwa kipigo cha mbwa mwizi kama nilivyo mfanya mwenzie Mada Maugo
kwani na yeye alikuwa anachonga sana lakini mwisho wa siku nikachukuwa ubingwa kupitia kwake yeye mana mpambano huu nilikuwa nausubili kwa hamu kubwa sana leo kesho
mbali na majeraha haya napenda kuwashukuru baadha ya watu walionisaidia  katika tukio zima la mimi kupata ajari na kunisaidia kutoa gari bondeni mpaka sasa ipo katika mikono salama ingawa imearibikwa kwa sababu ya kubondeka
mbali na hivyo nashukuru  promota Ally Mwazoa kwa kuwa na moyo wa huruma na kuhamua kusogeza mbele mpambano huo mpaka siku utakapotangazwa tena pia naomba watanzania waniombee duwa kwani naenderea vizuri kutibu majeraha yangu 











Bondia Thomasi Mashali akionesha majeraha aliyoyapata baada ya kupata ajali hivi karibuni picha nawww.superdboxingcoach.blogspot.com
JERAHA LINALO ONEKANA MKONONI
Bondia Thomasi Mashali akionesha majeraha aliyoyapata baada ya kupata ajali hivi karibuni picha nawww.superdboxingcoach.blogspot.com
THOMAS MASHALI
Bondia Thomas Mashali wa tatu kushoto akiwa na baadhi tya ndugu na jamaa akiuguza majeraha ya vidonda baada ya kupatas ajari hivi karibuni picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Thomasi Mashali akionesha majeraha aliyoyapata baada ya kupata ajali hivi karibuni picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
 
© 2012. Design by Ernest James Siwigo Chambasi - Supported By John James Chambasi And Maganza Family