PIGO KUNDI LA UCHEKESHEJI LA FUTUHI:MZEE DUDE WA FUTUHI AFARIKI DUNIA

Msanii wa tasnia ya uchekeshaji toka kundi la FUTUHI linalo rusha kazi zake kupitia Star TV, Mzee Dude amefariki dunia leo mida ya saa 11 jioni akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa Bugando ya jijini Mwanza ambako alilazwa mara baada ya kuzidiwa ugonjwa wa muda mrefu aliokuwa nao kwa figo kushindwa kufanya kazi.
Enzi za uhai wake Mzee Dude alikuwa mchezhi na mbunifu wa hali ya juu kuwavunja watu mbavu.
Mzee Dude atazikwa kesho jijini Mwanza majira ya alasili na taarifa kamili utazipata hapa.
 
© 2012. Design by Ernest James Siwigo Chambasi - Supported By John James Chambasi And Maganza Family