Kutoka kushoto ni wanamuziki: Joh Makini, Peter Okoye, Profesa Jay, Paul Okoye, Ben Pol na Lady Jaydee baada ya kuongea na wanahabri leo katika Hotel ya Kilimanjaro Hyatt Regency tayari kwa shoo ya kesho.
Kundi la P-SQUARE lililotua jana nchini Tanzania kutoka Nigeria kwa ajili ya tamasha kubwa litakalofanyika kesho Leaders Club wameahidi kutoa burudani yenye kiwango cha juu kwa Watanzania wote watakaohudhuria.
Wasanii hao mapacha kesho watapanda jukwaani na kupiga muziki wa live na bendi kwa mfululizo wa masaa zaidi ya mawili huku wakipewa shavu na wanamuziki Lady Jaydee, Professa Jay, Joh Makini na Ben Pol.
Tamasha hilo kubwa la muziki kwa mwaka huu, linatarajiwa kuanza saa 1 jioni bila kuchelewa.
(Chanzo: East Africa Radio Facebook Fan Page)
