![]() |
BENDI
za Twanga Pepeta, Msondo Ngoma na wanamuziki kibao kutoka Sikinde ni sehemu ya
wasanii watakaosindikiza tamasha kubwa la Gurumo 53 litakalofanyika mwezi huu.
Tamasha
hilo ambalo ni mahsusi kwa ajili ya kumuaga mwimbaji mkongwe Muhidi Maalim
Gurumo (pichani) litafanyika Jijini Dar es Salaam katika viwanja vya TCC Club Chang’ombe
Jumamosi Desemba 14, 2013.
Kwa
mujibu wa kamati ya watu sita inayoratibu tamasha hilo, Gurumo anaagwa baada ya
kutangaza rasmi kuachana na muziki wa jukwaani baada ya kudumu kwenye kazi hiyo
kwa miaka 53.
Mratibu
wa kamati hiyo Juma Mbizo amesema kutakuwa pia na wasanii wa bongo fleva,
vichekesho na sarakasi. Aidha
Mbizo amesema tamasha litatanguliwa na bonanza la soka la maveterani.
Hadi
kustaafu kwake Gurumo aliyezitumikia pia bendi za Kilimanjaro Chacha,Rufiji
Jazz, Kilwa Jazz, Sikinde na OSS – Ndekule, alikuwa ni kiongozi na mmoja wa
wamiliki wa Msondo Ngoma ambayo hapo awali ilijulikana kwa majina ya NUTTA,
Juwata na OTTU. Gurumo ameitumika Msondo katika majina yote ya nyuma.
Wasanii
waliowahi kuitumikia Sikinde ambao watakuwepo kumsindikiza Gurumo ni pamoja na
Cosmas Chidumule, Abdallah Gama, Hussein Jumbe, Mashaka Shaaban, Kalamazoo,
Henry Mkanyia na Karama Legesu. Wengine ni Ali Yahaya na Boniface Kachala,
Benno Villa Anton, Tshimanga Kalala Assossa na Ibrahim Mwinchande.
Baadhi
ya wasanii wengine watakaotumbuiza ni Komandoo Hamza Kalala, Kassim Mapili,
Hafsa Kazinja na Waziri Ali.
Kamati ya Gurumo iko chini ya uenyekiti wa Asha Baraka, makamu ni Waziri Ali na katibu ni Said Mdoe huku mratibu akiwa Juma Mbizo, wajumbe ni Said Kibiriti na Richardson Sakala. |
Habari kubwa Magazetini Kenya leo March 3, 2025
8 months ago

