
Elimu
ya Tanzania iliingia kwenye headlines siku kadhaa zilizopita baada ya
kutangazwa kwamba hakutakua na division zero na badala yake kutakua na
division five kwa Wanafunzi wanaomaliza elimu ya sekondari.
November 4 2013 Naibu waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi Philiph
Mulugo ameongea na XXL ya Clouds FM na kusema ‘taarifa zilizotolewa
awali zilikosewa kidogo kutokana na mkanganyiko sababu ishu ilikua bado
iko kwenye mjadala lakini nataka nikuhakikishie kwamba kutakua na
division 1, 2, 3, 4 na kutakua na division zero kama kawaida,
haijaondolewa’
‘kinachofanyika tu hapa ni zile point kutanuka baada ya kutoa yale
madaraja zile alama kurundikana sehemu moja, tumezihamisha angalau alama
zipishane alama 10 mpaka 15 kwa hiyo F itakua ni 0-19 na daraja jingine
lililoongezeka pale ni E ambalo 20-29 alafu daraja la D kutakua alama
30 -39, C ni 40 mpaka 49, B ni 50 mpaka 59, B+ ni 60 – 74 alafu A ni 75
mpaka 100′ –
Naibu waziri Philiph Mulugo
‘Nimeona wadau wengi wanacomment kwenye vyombo vya habari na kwenye
mtandao kwamba tumeshusha viwango vya ufaulu, hatujashusha ufaulu ila
tumesema tuyaweke haya madaraja kama ni ngazi, swala sio Wanafunzi wote
waende form IV lakini kuna vyuo vingine watu wanaweza kwenda kuchukua
ujuzi mwingine wa kujishughulisha ila tuwatambue kwamba wamepata alama
hizi hapa, anaepata F ambae ni 0-19 ajitambue kwamba hata cheti hawezi
kupata, watakaopata cheti ni E na D lakini hawatokua na uwezo wa neno
kwamba amepata au amefaulu japo watakua wanaekewa alama zao’ – Philiph
MulugoKwa kumalizia Mulugo anasema ‘zamani kulikua kuna A, B, C, D, F lakini sasa kuna A, B+,B, C, D, E na F ukijumlisha zile point zote unakuta mpaka mwishoni kabisa mtu ambae amepata F zote 7 katika masomo ya baraza la mitihani anakua na alama 49 ambayo tunasema huyu kapata 0 division ambayo ndio ilileta mkanganyiko kwa Watanzania na kusema ndio imeitwa division 5, hapana itaendelea kuitwa bado division zero hivyohivyo.
