Mkurugenzi
wa Elimu ya juu, Wizara ya Elimu na mafunzo ya Ufundi, Profesa Sylvia
Temu ambaye alikuwa mgeni rasmi aliyemwakilisha Waziri wa Elimu na mafunzo ya Ufundi akitoa hotuba yake wakati
wa uzinduzi wa mpango wa utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wanaosoma
vyuo vya nje ya nchi uliofanyika jana katika hoteli ya Serena jijini
Dar es Salaam.
Kaimu
Katibu mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania, Profesa Magishi
Nkwabi Mgasa akiwapongeza kampuni ya Global Education Link kwa
kushirikiana na Benki ya Afrika (BOA) kwa kuweza kubuni njia
itakayowawezesha wanafunzi wengi waliokuwa wanapenda kwenye kusoma nje
ya nchi ila wanakosa pesa. Vile vile aliwaomba wanafunzi kuacha
kukurupukia vyuo vya nje bila kutambua kama vinatambulika Tanzania ama
lah ili kuwaepushia usumbufu. Uzinduzi huo ulifanyika jana katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Naibu
katibu mkuu Tamisemi, Zuberi Samataba akiongea machache katika
uzinduzi wa utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wanaosoma vyuo vya nje ya
nchi uliofanyika jana katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji na mwanzilishi wa taasisi ya Global Education Link, AbdulMalki Molel akitoa maelezo jinsi mpango wa utoaji
wa mikopo kwa wanafunzi wanaosoma vyuo vya nje ambapo jna ilikuwa
ndiyo uzinduzi katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Afrika Tanzania, Ammish OWUSU-AMOAH akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi
wa mpango wa utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wanaosoma vyuo vya nje
ya nchi uliofanyika jana katika hoteli ya Serena jijini Dar es
Salaam.
Mmoja
ya wazazi waliohudumiwa na taasisi ya Global Education Link wakitoa
ushuhuda wao jinsi watoto wao walivyowezeshwa kutafutiwa nafasi za
masomo kwa vyuo vya nje ya nchi bila usumbufu kwa vyuo
vinavyotambuliwa na Tume
ya Vyuo Vikuu Tanzania. Ambapo wazazi hao walitoa rai yao kwa
wazazi wengine kuendelea kuiunga mkono GEL ili isonge mbele zaidi
kwa vile inafanya kazi zake kiuhakika bila ya kudanganya.
Waliongeza kuwa kwa
sasa wanafunzi wengi wamekuwa na moyo wa kusoma nje ila kuna baadhi
ya makampuni ambayo yamekuwa yakiwadanganya na kujikuta
wakidondokea kwenye vyuo ambavyo havitambuliki mwisho wake kuishia
kupoteza hela na muda. Uzinduzi huo ulifanyika jana katika hoteli ya
Serena jijini Dar es Salaama.
Mkurugenzi
wa Elimu ya juu, Wizara ya Elimu na mafunzo ya Ufundi, Profesa
Sylvia Temu ambaye alikuwa mgeni rasmi aliyemwakilisha Waziri wa Elimu na mafunzo ya Ufundi (katikati) akizindua. Pembeni toka kulia ni Wafanyakazi wa GEL, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Afrika Tanzania, Ammish OWUSU-AMOA, Kaimu
Katibu mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania, Profesa Magishi
Nkwabi Mgasa pamoja na Naibu katibu mkuu Tamisemi, Zuberi Samataba.
Hiki ndicho kilichozinduliwa. Picha na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
