Mwanamuziki
maarufu wa kizazi kipya Hamisi Mwinjuma a.k.a Mwana Fa a.k.a Binamu
ambaye hivi sasa yuko nchini Marekani kwa ziara maalum anatarajiwa kuwa
mgeni katika kipindi cha Live Talk katika idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya
Amerika (VOA).
Kipindi hicho ambacho hurushwa moja kwa moja na radio washirika
kinaanza saa moja na nusu saa za Afrika Mashariki na saa kumi na mbili
na nusu jioni saa za Afrika ya kati na Washington itakuwa ni saa tano na
nusu asubuhi .
Katika
matangazo ya Ijumaa hii VOA itazungumzia suala zima la Muziki wa Bongo
Flava unakoelekea na changamoto zake kwa ujumla.
Kipindi hiki kitarushwa kwa muda wa saa moja ambapo nusu ya kwanza
itakuwa kwenye radio washirika na ili usikie kwa saa nzima ungana na
VOA kwenye mtandao . www.voaswahili.com

