![]() | |
Post ya Zitto Kabwe inaanzia hapa Dr. Willbrod Slaa : ” Hatuna tatizo hata kidogo na Zitto Kabwe. Huyu ni Naibu Katibu Mkuu wetu kama kuna tatizo jambo ambalo ameleta tutamaliza kwa mujibu wa taratibu na tutaendelea na kazi na umoja wetu” ” Waraka huo mchafu umeandikwa na viongozi wa CCM na kutoka idara nyeti ya serikali chama kitapata taarifa zao na kuanika majina yao na nafasi zao” Edwin Mtei : ” Haya mambo hayatubabaishi tunajua ni uongo uliotungwa ili kutugombanisha. Kesho unaweza kusikia Zitto amehongwa hiki au kile. Keshokutwa ukasikia Slaa amehongwa hiki baadaye Mbowe amefanya hivi lengo kutuvuruga” Mabere Marando: ”Andishi hili ni feki nimeliangalia andishi lote. Nimejiridhisha kwamba limetengenezwa na watu wasiotakia mema Chadema” Maneno mazuri sana yenye ukweli mtupu. Hata hivyo hekaya hii imesambazwa na wanachama wa CHADEMA na mmoja ni kiongozi wa mkoa na akaweka kwenye blogu yake. Viongozi wengine waka ‘like’ kwenye jamii forums. Hawa wametumwa na usalama na CCM? CHANZO-MILLARD AYO |
Habari kubwa Magazetini Kenya leo March 3, 2025
8 months ago

