| WATU wanane wamepoteza maisha katika matukio mawili tofauti
yaliyotokea jana mkoani Pwani, wakiwamo waendesha pikipiki watano
waliogongana na lori. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Kamishina
Msaidizi Mwandamizi (SACP), Ulrich Matei, alisema tukio la kwanza
lilihusisha waendesha bodaboda watano, waliofariki katika ajali. Kwa mujibu wa Kamanda Matei, ajali hiyo ilitokea saa 2 usiku eneo la Ruvu Darajani Kata ya Vigwaza baada ya waendesha bodaboda kugongana na tela lenye namba za usajili T.602 ACT la lori lenye namba T.493 ABP aina ya Scania, lililokuwa likiendeshwa na Dastan Migunda (35), mkazi wa Kitunda Dar es Salaam. Aliwataja waliopoteza maisha kuwa ni Saidi Dosa (17), Severine Luoga (19), Philemon Job (20), Nassoro Mzalamila (18) na Sadam Mapunda (21). Kamanda Matei alisema ajali hiyo imetokana na mwendo kasi wa waendesha pikipiki watatu waliokuwa wakitokea Picha ya Ndege kwenda Kijiji cha Buyuni kumfuatilia kijana aitwaye Ramadhani Rajabu (16), dereva wa bodaboda eneo la Kwa Mathias, aliyetuhumiwa kwa wizi wa Pikipiki yenye namba.T 216 CNC aina ya Sanlg. “Miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya Tumbi Kibaha ikisubiri kufanyiwa uchunguzi wa Daktari,” alisema. Katika tukio lingine, Matei alisema majira ya saa 8:50 mchana eneo la Kibong’wa, wilayani Kisarawe watu watatu wamepoteza maisha baada ya kuporomokewa na udongo wakiwa wamejipumzisha chini ya machimbo ya kokoto. Matei aliwataja watu hao kuwa ni Mwazani Salehe (18), Ally Twaha (2) na Hasnatha Semin (mwenye miezi 5) wote wakazi wa Kibong’wa. “ Watu hao walikuwa wamepumzika katika eneo hilo na ndipo udongo ulipowaporomokea, katika tukio hilo Amina Emil (28) amejeruhiwa na kwa sasa amelazwa katika Hospitali ya Wilaya Kisarawe akiendelea kupatiwa matibabu,” alisema. |
Habari kubwa Magazetini Kenya leo March 3, 2025
8 months ago
