HABARI JUU YA KIFO CHA DKT SENGONDO MVUNGI

Sengondo Mvungi 1
Ni juzi  tu ambapo Waziri wa mambo ya ndani Dr. Emmanuel Nchimbi alitangaza kushikiliwa kwa watu tisa wanaotuhumiwa kuhusika na ujambazi uliofanywa dhidi ya Dr. Sengondo Mvungi aliekua mjumbe wa Tume ya Marekebisho ya Katiba Mpya na kiongozi wa NCCR-Mageuzi.
Taarifa Zilizoenea hadi hivi sasa na kuthibitishwa Dr Mvungi amefariki dunia akiwa mahututi hospitalini nchini Afrika Kusini na  taarifa kutumwa nyumbani Tanzania ambapo wafanyakazi wenzake ofisi ya tume ya mabadiliko ya katiba wameambiwa wakae karibu na simu zao ili kikitokea chochote kingine wafahamishwe.
Tayari viongozi mbalimbali kama Mh. Warioba, Katibu wa tume, naibu na watumishi wengine wachache wamekwenda nyumbani kwa marehemu.

Hizi picha hapa chini ni za Wafanyakazi wenzake baada ya kupata taarifa za msiba ofisini.
kifo cha Sengondo Mvungi Nov 12 2013 2
kifo cha Sengondo Mvungi Nov 12 2013
 
© 2012. Design by Ernest James Siwigo Chambasi - Supported By John James Chambasi And Maganza Family