
Katika kuelekea ufunguzi wa mgahawa wao magwiji wa soka wa klabu ya Manchester United Ryan Giggs na Gary Neville jana waliingia kwenye mashindano ya kupika misosi. (HM)
Giggs na Neville kwa pamoja jana walishiriki kwenye mashindano hayo yaliyofanyika maeneo ya Westfield Stratford City shopping centre jijini London ikiwa ni moja ya shamrashamra ya ufunguzi wa mgawaha wao wa Cafe Football.
Wawili hao walishindana na mpishi mkuu wa mgahawa huo, Brendan Fyldes pamoja na mpishi wa Michelin chef Michael Wignall.
Giggs na mwenzie walipika vyakula
vikuu vitatu ambavyo vitakavyokuwa vikipatikana hapo vikiwemo Nev's
Noodle Pot, Wignall's Halftime Orange na Chocolate Pistachio Turf.
Neville alisema: 'Shindano hili
lilikuwa nafasi nzuri kwa wanunuzi Westfield Stratford City kuona nini
tumewaandalia kwenye Cafe Football.'Mapishi matatu tuliyopika ni mfano
tu uzuri wa vyakula ambavyo vitakuwa vikipatikana Cafe Football. Chanzo:
shaffihdauda
