Akielezea Mkasa Huo Kupitia Interview Yake Aliyofanya Na Mwandishi Wa Habari Kutoka Kituo Kimoja Maarufu Cha Habari Nchini ( Clouds Media Group ) Bwana Millard Ayo Kupitia Channel Yake Ya YouTube Aliyoiita Ayo Tv,Mahojiano Yao Yalikua Kama Ifuatavyo
Ney wa Mitego : ‘Ni kweli ilitokea unajua unapofanya kitu sometime unatakiwa uvae uhalisia kabisa wa kitu ili tusionekane tuna-fake sana, kweli kwenye video yangu ya Salam zao kuna watu ambao nimewavalisha nguo zinazoendana na za polisi ambapo tukiwa katika harakati za kufanya video askari wakaingilia kati eti hatuna kibali na hatukuruhusiwa kufanya vile’
‘Kikubwa nilichosema ni kwamba hizi sio nguo za polisi, tupo kwenye kazi ambayo inahitaji kuonyesha uhalisia wa kitu ambacho tunakifanya, muonekano tu ni kama wa polisi lakini hakuna nguo ambayo ni direct hii ni nguo ya polisi, mwisho wa siku maelewano yalikuwa ni madogo ikabidi tufikishane mpaka kituoni, bahati nzuri namshukuru mwenyezi Mungu kwa hapa aliponifikisha hata wakubwa pia wananielewa nikieleza kitu au kuniona niko mahali fulani na kuweka kipaumbele na kusema haiwezekani.
AyoTV : Ilikuaje mpaka ukakamatwa na ulikuwa kwenye mazingira gani na wapi?
Ney wa Mitego : Ilikuwa ni Magomeni Kagera tulikuwa kwenye mazingira ya ku-shoot tayari, tulikuwa tumesha-shoot kama clip mbili tatu ambapo kuna clip ambayo tulikuwa tunakimbizana nafikiri ile ndiyo ilileta mushkeli kwasababu tuliingia mtaani… Wananchi nao walishtuka kuona kile kitu unajua Kagera, Manzese yote ni nyumbani kwangu sehemu zote zile mimi nimeishi kwa hiyo tulivyoingia wananchi wakatulia.
‘Askari walivyokuja wakasema hiki mnachofanya kibali kipo wapi, nikawambia tena vitu kama hivi hadi tuombane vibali wakasema hao mbona wamevaa nguo za polisi, nikawambia hizi sio nguo za polisi zinafanana tu lakini kama unavyojua askari hawana dogo ikabidi tupelekane polisi tukakaa tukaya solve yakaisha.
AyoTV : Umekaa polisi kwa muda gani?
Ney wa Mitego : ‘Kusema kweli ni kama dakika kumi na tano hivi kwasababu mkubwa mwenyewe hakuwepo bahati nzuri mkubwa alifika kama baada ya dakika 15 na kwa kuwa mimi ni mtu wa dezain hii kila mtu akawa amejua mimi nimepelekwa pale, tukaongea nikamwambia tatizo ni video,mwisho tukayamaliza.
AyoTV : Walikufanya chochote walivyokukamata?
Ney wa Mitego : Sikufanywa chochote unajua huwezi kubishana na serikali, nilifata kile walichotaka nikifanye kwa muda ule pia niliwaambia kile mimi sitaki kufanyiwa kwa muda ule kwasababu nilikua kwenye kazi na mimi ni mtanzania ambaye naruhusiwa kufanya chochote ikiwa tu sio cha uhalifu.
AyoTV : Ulipigwa pingu?
Ney wa Mitego : Swala la pingu mimi nilikataa kufungwa kwasababu mimi sijaua mtu, sijaiba, sijavunja japokuwa sometimes wakishamuona star wanakuwa wanataka sifa, walitaka kuleta hizo lakini kwangu ilikuwa tofauti hata maaskari wenyewe walikuwa wananikamata walikua wanajua nini nafanya ila sijui ilikuwa ni nini pale.
AyoTV : Video yako ya ‘Salam zao’ inatoka lini?
Ney wa Mitego : Video yangu ya Salam zao panapo majaaliwa Ijumaa itakuwa released kwenye mitandao yote na TV zote na mara ya kwanza kupitia AyoTV na millardayo.com watu watapata kuiona ikiwa ni exclusive., pia naomba niongee kitu kimoja ambacho sitakiwi kusahau, nimekuwa nominated kwenye tuzo za Nzumari…… endeleeni kunipigia kura kwenye nyimbo yangu ya muziki gani ili tarehe 23 nipate tuzo za wimbo bora wa Afrika mashariki na mwanamuziki bora wa kiume kutoka Tanzania.

