Japokuwa bado yupo kwenye probation lakini Chris Brown bado
anaendelea kuvunja sheria za huko Marekani. Sources mbalimbali kutoka
kwenye mitandao ya uhakika huko zinasema kwamba Chris amekamatwa pamoja
na bodygurd wake baada ya Chris mwenyewe kumpiga ngumi ya uso na
kumvunja pua jamaa mmoja waliyekutana kwenye hotel.
Habari juu ya tukio hilo linasema kwamba wasichana wawili walikuwa
wanapiga picha na Chris Brown na wakati huohuo jamaa huyo alijaribu
kwenda kwa nyuma na kuharibu picha hiyo (Photoboom). Chris Brown
alivyomuona ndio hasira zake zikamfanya amrushie ngumi ya uso na kumpata
puani.
Watu wakaribu na Chris Brown wametoa habari tofauti juu ya tukio hili
na kusema kwamba huyo jamaa alikuwa anajaribu kupanda tour bus la Chris
Brown lakini alizuiwa. "Alitaka kupanda baada ya wasichana
wengine kukataliwa sasa katika harakati za kuzuiwa asiingie ndio
aliumia puani"walisema

