![]() | ||
| T.I.D |
![]() | |
| Ommy Dimpozi Azidi Kuandamwa Na Kinachosadikiwa Na Kusemekana Amemtusi Marehemu Albert Mangwair,Kisa Hicho Kiliripotiwa Na Moja Ya Magazeti Maarufu Nchini Hapa,Nanukuu Kama Kilivyoandika:- |
CHANZO A
"Ommy alidhihaki hata ushiriki wa
wanamuziki waliosimamisha shughuli zao kwa muda kisha kuungana na
kushikamana kuhakikisha Ngwair anazikwa kwa heshima.
“Sitaki nikifa yatokee kama ya Ngwair, amekufa Afrika Kusini, hata kuusafirisha mwili kuuleta Tanzania imebidi mpaka watu wachangie, ile ni aibu sana,” alisema Ommy kwa dharau."BONYEZA HAPA KUSOMA ZAIDI KUTOKA KWENYE CHANZO CHETU"

CHANZO B
JUMANNE (JUNI 11)
Kutokana na uzito wa maneno ambayo Ommy aliyatamka kuhusu Ngwair, siku iliyofuata (Jumanne), mwandishi wetu alimpigia simu kumuuliza kama maelezo hayo ya kashfa aliyatoa akiwa amelewa au la?
Ommy kwa kujiamini, alijibu kwamba alichokisema kuhusu Ngwair ni ukweli kwa asilimia 100.
MWANDISHI: Nakushauri kama mdogo wangu, siku nyingine usirudie kutamka maneno hayo ni mabaya sana kwa mtu aliyekufa.
OMMY: Sijaongea neno baya, nimesema ukweli wasanii hatutakiwi kufa maskini.
MWANDISHI: Wewe unaona mtu akichangiwa baada ya kufa ndiyo kipimo cha umaskini?
OMMY: Kuna mambo mengi ambayo yangefanyika kabla ya kuchangiwa lakini Ngwair alishindwa kuyafanya.
MWANDISHI: Sasa Ngwair angefanya nini wakati yeye ameshakufa?
OMMY: Kuna mambo yangefanyika, mfano kusafirisha mwili kutoka Afrika Kusini.
MWANDISHI: Sasa Ngwair angejisafirisha mwenyewe?
OMMY: Nachosema mimi ni kwamba wasanii hatutakiwi kufa maskini.
MWANDISHI: Sikiliza Ommy, hata mabilionea wakubwa huwa wanachangiwa. Mtu kuchangiwa siyo kashfa wala aibu kama unavyotaka kulionesha tukio la Ngwair. Marehemu Steven Kanumba alikuwa anatembelea Toyota Lexus V8, mbona alipokufa kila kitu alifanyiwa? Ni jambo la kawaida.
OMMY: Ngwair alikuwa na ‘stresi’ za maisha ndiyo maana alikuwa anakula unga.
MWANDISHI: Ulishawahi kumwona Ngwair akitumia unga?
OMMY: Kwanza nakusikia unanirekodi, sijui una malengo gani.

CHANZO C
Juni 8, mwaka huu, katika Ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam, wakati
wa utoaji wa Tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards (KTMA) mwaka
2012-2013, Ommy Dimpoz alizungumza maneno ya kashfa ambayo moja kwa moja
yalitafsiriwa ni dongo kwa Ngwair.
Baada ya kutangazwa mshindi wa kipengele cha Video Bora ya Mwaka na kukabidhiwa tuzo yake, Ommy alibwabwaja: “Jamani tumechoka kuzika wasanii maskini wenye majina makubwa.”
Japo hakutaja jina la yule aliyekuwa anamzungumzia, tafsiri ya wengi ni kwamba Ommy alikuwa anamzungumzia Ngwair kwa sababu ndiye staa aliyekuwa amezikwa kishindo cha siku moja tu kabla ya usiku huo wa tuzo. Ngwair alizikwa Alhamisi, tuzo Jumamosi.
“Huyu dogo ana nyodo sana, sasa haya ni maneno gani ya kuzungumza? Hapa anamzungumzia Ngwair, ila anapaswa kujua kwamba yeye bado msanii mdogo sana kumlinganisha na Ngwair,” alisema mtangazaji mmoja kwa masikitiko.