 |
Mwanadada Judith Mbibo aka Lady Jaydee usiku wa kuamkia Jumamosi ya
June 15 amefanikiwa kuweka historia kwenye muziki wa Tanzania kwa
kulijaza eneo zima la Nyumbani Lounge alipokuwa akifanya show yake ya
kuadhimisha miaka 13 tangu aanze muziki.
Hii imedhihirisha kuwa majina
anayojiita mwanadada huyu ni ya halali kabisa na yanamfaa kwani tafauti
na watu walivyodhan palijaa watu hadi wakaanza kubebana ama kwa hakika
huyu ni komando,anaconda hebu anagalia picha mdau utakubaliana na mimi.. PICHA KWA HISANI YA BONGO 5 | |
Wadau
mbali mbali wa muziki hapa nchini wapo ndani ya ukumbi huu kusuhudia
show hii ambayo ilikuwa ikisubiriwa kwa hamu na wapenzi wa
muziki.
Ndani
ni nyomi la hatari,lakini nje nako watu bado wanataka kuingia huku
wengi wao wakisema kuwa "hata kama hakuna siti,sie tuko radhi kusimama
ilimradi tumsapoti Dada yetu."
Foleni bado ni ndefu na watu bado wanazidi kuingia ukumbini hapa hivi sasa.
Katika show hiyo, Lady Jaydee amesindikizwa na wasanii mbalimbali
wakiwemo Juma Nature, Sugu, Profesa Jay, Wakazi, Grace Matata na
wengine. Pia Jaydee ameitumia siku hiyo kuzindua albam yake mpya,
Nothing But The Truth na kusherehekea siku yake ya kuzaliwa. Hizi ni
picha za show hiyo.