Dar es Salaam. Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA)
imewapiga marufuku wafanyabiashara wa dawa na vipodozi wanaouza kwenye
vyombo vya usafiri na kuwataka kuacha mara moja kwani kufanya hivyo ni
kuvunja sheria.
Wananchi pia wametakiwa kuacha kununua bidhaa hizo
kwenye vyombo vya usafiri kutokana na ubora na usalama wake kuwa wa
shaka na matumizi yake ni hatari kwa afya.
Katika taarifa iliyotolewa
na TFDA kwenye vyombo vya habari jana, ilieleza kuwa kumekuwa na tabia
ya wafanyabiashara wadogo kuuza bidhaa aina ya dawa katika vyombo vya
usafiri hasa treni na mabasi ya abiria ambapo ni kinyume cha sheria.
Kwa
mujibu wa taarifa hiyo inaeleza kuwa dawa na vipodozi ni bidhaa
zinazotengenezwa na kemikali zenye sumu zinazodhibitiwa na TFDA ambapo
baadhi ya bidhaa zinatakiwa ziuzwe na kuhifadhiwa katika maeneo ambayo
yanakidhi matakwa ya uhifadhi na uuzaji.
Ilieleza kuwa bidhaa hizo
zikihifadhiwa katika maeneo yenye joto jingi, pachafu na pasipo na
uangalizi wowote zinakuwa duni, kushindwa kutibu na kutengeneza sumu
zinazoweza kumwathiri m tumiaji.

|