MADRID WAICHAPA GALATASARAY BAO 3-0


Up and over: Cristiano Ronaldo scored the first against Galatasaray at the Santiago Bernabeu
KLABU ya Real Madrid imejiweka kwenye nafasi nzuri ya kwenda Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya usiku wa jana kuilaza Galatasaray mabao 3-0 kwenye Uwanja wa Bernabeu.
Cristiano Ronaldo alifunga bao la kwanza mapema kipindi cha kwanza dakika ya tisa kabla ya Karim Benzema kufunga la pili dakika ya 29. 
Gonzalo Higuain aliyetokea benchi kipindi cha pili alifunga la tatu kwa kichwa dakika ya 73 na kuwafanya Madrid waende kwenye Uwanja wa Turk Telecom Arena Jumanne ijayo kifua mbele.
Didier Drogba aliyeiongoza Chelsea kutwaa taji hilo la Ulaya msimu uliopita, jana alipatya nafasi mbili nzuri lakini akashindwa kuzitumia.
Katika mchezo huo, kikosi cha Real Madrid kilikuwa: Diego Lopez, Varane, Ramos, Coentrao, Khedira, Ronaldo, Ozil/Modric dk80, Alonso, Essien, Di Maria/Pepe dk86 na Benzema/Higuain dk65.
Galatasaray: Muslera, Dany Nounkeu, Kaya, Eboue, Altintop/Bulut dk78, Inan, Felipe Melo, Riera/Amrabat dk83, Sneijder/Zan dk46, Yilmaz na Drogba.
Katika mchezo mwingine jana, Malaga na Borussia Dortmund zilitoka sare ya bila kufungana.


Kitu na boksi: Cristiano Ronaldo akifunga bao la kwanza dhidi ya Galatasaray Uwanja wa Santiago Bernabeu
Up and over: Cristiano Ronaldo scored the first against Galatasaray at the Santiago Bernabeu
In the goals: Karim Benzema got the second for the hosts
Karim Benzema akishangilia bao lake
Struggle: Didier Drogba led the line for the visitors
Malalamiko: Didier Drogba akilalamika
Three and easy: Gonzalo Higuain scored the third with a glancing header
La tatu kiulainiii: Gonzalo Higuain alifunga bao la tatu kwa kichwa
Three and easy: Gonzalo Higuain scored the third with a glancing header
  Mpambano wa wanaume: Sergio Ramos (kushoto) akipambana na Didier Drogba kipindi       cha pili jana ambaye alianguka kama anavyoonekana picha ya chini
Rough and tumble: Sergio Ramos (left) drags Didier Drogba to the floor in the second half
Over you go: Ronaldo hits the deck after Semih Kaya (centre) backs into the Portugal forward
                  Mpiganaji: Ronaldo akipambana dhidi ya wachezaji wa Galatasaray
 
© 2012. Design by Ernest James Siwigo Chambasi - Supported By John James Chambasi And Maganza Family