KAMA ULIMISS HABARI NA PICHA YA MWILI WA DEREVA WA BAJAJI ANAYESEMEKANA AMEUWAWA NA MWANAJESHI KAWE HII HAPA




MWILI WA MAREHEMU YOHANA MDA MCHACHE BAADA YA KUUAWA NA WANAJESHI WA JWTZ.


 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela.

Askari anayedaiwa ni wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)  anadaiwa kuua dereva wa bajaj kwa kutumia bunduki katika maeneo ya Kawe Shoko, jijini Dar es Salaam.

Tukio la kuuawa kwa kijana huyo jana jioni inadaiwa lilitokana na  kutokea  mabishano kati yake na mwanajeshi huyo wakati ikipita eneo ambalo raia hawaruhusiwi kupita.

Vurugu kubwa zilitokea katika eneo hilo baada ya kutio hilo huku vijana wenzake marehemu kukusanyika kuhoji sababu za kuawa kwa mwenzao.

Mashuhuda walisema kuwa baada ya askari kuho kumpiga risasi kijana huyo na kumuua, mwili wake ulichukuliwa na gari la kubebea wagonjwa na kukimbizwa katika Hospitali ya Jeshi ya Lugalo. 
SOURCE AUDIFACEJACKSON BLOG
 
© 2012. Design by Ernest James Siwigo Chambasi - Supported By John James Chambasi And Maganza Family