PICHA MSIBANI NYUMBANI KWA MAREHEMU OMARY OMARY

Ndugu na jamaa wakiwa na majonzi msibani kwa marehemu Omar Omar, Temeke-Mikoroshini jijini Dar.


Marehemu Omar Omar enzi za uhai wake.


Dada wa marehemu (hakufahamika jina lake mara moja) akiwasiliana na ndugu wengine ambao hawapo msibani.




Mwanamuziki wa kizazi kipya, Dully Sykes, mwenye T-shirt  ya mistari (nyuma katikati) akibadilishana mawazo na wazee msibani hapo.


Meneja wa marehemu, Bonga Ticha (kushoto) akiwa na meneja wa kundi la muziki la Wanaume Family, Mkubwa Fella.



Baadhi ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya na mameneja wao wakiwa msibani hapo.
WAOMBOLEZAJI mbalimbali wakiwemo wasanii wa muziki wa kizazi kipya, leo wamekusanyika nyumbani kwa mwanamuziki mkongwe wa miondoko ya mnanda, Omar Omar Mfungilo, aliyefariki dunia usiku wa kuamkia leo nyumbani kwao Temeke-Mikoroshini, Dar es Salaam. Kwa mujibu wa baba mdogo wa marehemu, mzee Yusufu Ally Mfungilo, marehemu Omar anatarajiwa kuzikwa LEO saa saba mchana huko Temeke.                                            
                                                    (PICHA NA ISSA MNALLY / GPL)
 
© 2012. Design by Ernest James Siwigo Chambasi - Supported By John James Chambasi And Maganza Family