MBUNGE
wa Ubungo John Mnyika, ametaja majina ya watu 16 ndani ya Shirika la
Umeme Tanzania (Tanesco) ambao amewahusisha na ufisadi ndani ya shirila
hilo la umma. Mnyika
ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Madini na Nishati alisema watu hao ndio
wanaoshirikiana kuihujumu Tanesco na kuliingiza taifa katika hasara.
Kati ya majina hayo ambayo ameyaita kuwa ni ya awamu ya kwanza wamo baadhi ya waliokuwa watendaji wa shirika hilo ambao wamesimamishwa kupisha uchunguzi unaofanywa na Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG).
Kati ya majina hayo ambayo ameyaita kuwa ni ya awamu ya kwanza wamo baadhi ya waliokuwa watendaji wa shirika hilo ambao wamesimamishwa kupisha uchunguzi unaofanywa na Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG).
Alipoulizwa
wiki iliyopita kuhusu uchunguzi huo, GAG Ludovick Utouh alisema
uchunguzi huo umeshakamilika na kilichokuwa kikisubiriwa ni kuikabidhi
ripoti hiyo kwa bodi ya Tanesco.
Mnyika
aliwataja vigogo wengine watatu wa Tanesco na kueleza kuwa walifanya
uzembe na kushindwa kusimamia sheria ya ununuzi wa umma na kupendekeza
kampuni mbili kupewa zabuni, licha ya kuwa hazikutimiza masharti kwa
sababu ya mgongano wa maslahi.
Mnyika alipendekeza vigogo hao kuchukuliwa hatua za kinidhamu.
Aliwataja watumishi wawili ambao
walishindwa kutoa taarifa za ukiukaji wa vigezo vya utoaji wa zabuni
namba PA/001/09/HQ/W/014 na kufanya kampuni moja kati ya hizo mblii
kupewa zabuni.
Alisema watendaji hao walichangia
kufanya kampuni hiyo kupewa zabuni pamoja na kwamba haikuwa na fedha na
kuiwezesha kupewa malipo ya asilimia za ziada kinyume na mkataba.
Akapendekeza watendaji hao kuchuliliwa
hatua za kinishamu. nMnyika aliwataja watumishi wengine sita wa Tanesco
ambao kwa pamoja walifanya uamuzi uliosababisha kutolewa kwa mkataba
namba PA/001/HQ/W/14 wa Machi 11,2010 kwa kampuni hiyo bila kuzingatia
uwezo wa kitaalam, kifedha na hivyo kukiuka sheria ya ununuzi wa umma.
Alisema hao wanatakiwa kuchukuliwa hatua ili kuwadhibiti watumishi wa umma wanaoliingiza taifa katika mikataba mibovu.
Mnyika katika taarifa yake hiyo
aliwataja wafanyakazi watatu wa Tanesco akieleza kuwa walihusika katika
kutoa mapendekezo yaliyowezesha kampuni ya McDonald kupewa mkataba wa
zabuni kinyemela.
Mnyika alipendekeza wachukuliwe hatua
za kisheria ili kuepusha Tanesco kuingia mikataba kuliongezea shirika
mzigo wa gharama na kusababisha ongezeko la bei ya umeme.