MAJAMBAZI WAVAMIA MSAFARA WA MAITI SINGIDA,WAPORA ZAIDI YA MILLIONI KUMI NA TISA NA KUSACHI JENEZA

 
Gari aina ya Land Cruiser mali ya chuo cha SUA cha mjini Morogoro kama linavyoonekana baada ya kupigwa mawe na watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi nje kidogo ya mji wa Singida.
---
Watu wasiofahamika idadi yao na ambao wanadhaniwa kuwa ni majambazi, wamevamia gari lililokuwa linasafirisha maiti kutoka Morogoro mjini hadi mkoa wa Mara na kupora zaidi ya shilingi milioni 19.8.

Baada ya kumaliza zoezi la uporaji huo, majambazi hayo yalishusha jeneza na kisha kulifumua na kuanza kulisachi.

Jeneza hilo lilikuwa limebeba mwili wa mwanafunzi Munchari Lyoba, mwanafunzi wa mwaka wa tatu aliyekuwa anasomea elimu ya biashara kwenye chuo cha SUA.

Amesema gari hilo lilibeba viongozi wa wanafunzi sita na viongozi wengine wanne akiwemo dereva.

Akizungumza na waandishi wa habari nje ya chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali ya mkoa wa Singida, mkuu wa msafara huo Makarang Nouna, amesema tukio hilo limetokea Disemba 6 mwaka huu saa 7.30 usiku, na lilihusisha gari Land Curise lenye namba za usajili SU 37012 na lilikuwa likiendeshwa na Kalistus Malipula.


Mhudumu wa chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya mkoa mjini Singida ambaye jina lake halikuweza kutambuliwa mara moja, akiliweka sawa jeneza baada ya kufanyiwa ukarabati baada ya kubomolewa na majambazi na kulisachi. (Picha na Nathaniel Limu).
---
Akifafanua zaidi, amesema kwa upande wake yeye ameporwa shilingi milioni mbili ambazo zilikuwa kwa ajili ya kugharamia msafara huo, jumla ya shilingi milioni 8.8 ambazo zilichangwa na wanafunzi kama rambi rambi kwa mwenzao, na shilingi milioni tisa ambazo wasindikizaji walikuwa nazo zikiwa ni posho.

“Pia tumeporwa simu zetu zote za mikononi, viatu, laptop na mabegi yote ya nguo zetu”amesema.

Makaranga ambaye amesema anafanya kazi za kiutawala katika chuo cha SUA, amewataja walioumizwa zaidi ni pamoja nay eye, dereva Malipula na kiongozi wa wanafunzsi Idd Idd na kutibiwa katika hospitali ya mkoa na kuruhusiwa.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Singida Mwalimu Queen Mlozi, ambaye aliwasiliana na uongozi wa SUA Morogoro kwa ajili ya shughuli ya kutuma gari jingine na ukarabati wa jeneza, amesema kuwa kwa ushirikiano wa jeshi la polisi na kamati ya ulinzi na usalama, watahakikisha watu waliofanya unyama huo, wanakamatwa mapema iwezekanavyo ili waweze kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria.
SOURCE:http://kajunason.blogspot.com/


 
© 2012. Design by Ernest James Siwigo Chambasi - Supported By John James Chambasi And Maganza Family