Rihanna ameshinda kesi yake dhidi ya duka kubwa la Topshop la nchini Uingereza lililokuwa likiuza T-shirts zenye picha yake. Mahakama ya rufaa ya jijini London imetoa katazo la kuuzwa kwa T-shirts hizo zilizokuwa zikiuzwa bila ridhaa ya Rihanna. Staa huyo aliishtaki kampuni mama ya Topshop, Arcadia kwa kudai fidia ya dola milioni tano mwaka 2013 kutokana na T-shirts hizo zenye picha yake iliyochukuliwa wakati akishoot video mwaka 2011. |