Hii ni mara ya kwanza kwa chanjo hii kupelekwa kwenye nchi iliyoathiriwa zaidi na Ebola. Lakini Wataalamu wanasema, wakati huu maambukizi ya Ebola yakiwa yanapungua,itakuwa vigumu kubaini kama chanjo hii inatoa kinga dhidi ya Virusi vya ugonjwa huo. Chanjo hii ilitengenezwa na Kampuni moja ya Uingereza, GlaxoSmithKline (GSK )na Taasisi ya kitaifa ya afya nchini Marekani GSK imesema ndege iliyo na dozi za awali takriban 300 za chanjo inatarajiwa kufika Monrovia siku ya ijumaa. Kampuni ina matumaini mtu wa kwanza kujitolea atapata chanjo hiyo wiki chache zijazo. Wanasayansi wanalenga kuwahusisha watu watakaojitolea takriban 30,000 katika majaribio hayo wakiwemo wafanyakazi wa afya. Ikiwa taratibu zote zitafuatwa, Watu 10,000 watapatiwa chanjo ya GSK. |