Moja ya timu za Majeshi – JKT Ruvu
Katibu
mkuu wa Shirikisho la soka nchini, TFF, Celestene Mwesiga amesema kuwa
kuanzia msimu ujao katika ligi kuu ya Tanzania hakuna mmliki mmoja
ambaye ataruusiwa kumiliki timu zaidi ya moja kama ambavyo Shirikisho la
soka Afrika, CAF na lile la ladunia FIFA walivyoagiza. Kwa maana hiyo
timu kama JKT Ruvu, JKT Mgambo, Ruvu Shooting ambazo zote zipo chini ya
umiliki wa jeshi la kujenga Taifa, zitapigwa mnada.
Sasa
mmliki wa timu hizo atatakiwa kuchagua ni timu gani ambayo ataaiuza au
kutengeneza kampuni mpya ya umiliki, na hazitaruhusiwa kucheza ligi kuu
endapo zitaendelea kuwa chini ya umiliki mmoja kuanzia msimu ujao.(P.T)
" Labda
kwa faida ya Watanzania ili kueleweka vyema, hili si agizo ambalo
limelenga timu za majeshi au timu za Polisi, ila ni zoezi la kutoa
leseni kwa vilabu, halijalenga klabu. Mojawapo wa msingi wa kutoa leseni
kwa klabu ni pamoja na kuepuka mtu mmoja kumiliki vilabu zaidi ya
kimoja. Siwezi kisema kama ni leo hilo suala litafanyika lakini, lakini
kila mshiriki, kila mdau ajue kabisa huko ndiko tunakoelekea. Kuanzia
msimu ujao vilabu vyote vitakavyoshiriki ligi vitatakiwa kuwa na leseni.
Huu ni utaratibu/maagizo ya CAF na FIFA ambao hawataki umiliki mmoja
kwa vilabu zaidi ya kimoja kwenye ligi moja."
Katika
kuonesha kuwa jambo hilo si la masihara TFF tayari imetoa taarifa kwa
vilabu vyote, sasa ni wakati wa wamiliki ambao wanafahamu wanamiliki
idadi ya timu zaidi ya moja kufanya utekelezaji wa utafutaji wa leseni
hiyo ya ligi kuu.
" Hili
linawahusu wamiliki wa bilabu vyetu au kokote pale Afrika kama kuna
mmiliki mmoja ambaye anajijua ana vilabu ni lazima atafute namna ambayo
umiliki huo utatenganishwa na kutokuwa chini ya mtu mmoja.
Litafanyilaje, uamuzi wa kwanza ni wamiliki wenyewe kuamua ataendelea
kuwa na timu ipi na ipi anaiuza au timu gani wataziunganisha"
Kuanzia
msimu ujao timu za Manispaa ( mfano Mbeya City) hatakuwa mbili hivyo
kutoa uwezekano wa timu kama Kuregenzi ya Mafinga kutocheza ligi kuu
endapo itapanda na kuendelea kuwa chini ya Manispaa. Jeshi la Polisi pia
litatakiwa kufanya uchaguzi wa timu ya kuendelea kumiliki kati ya rundo
la timu walizonazo. Polisi Morogoro ipo katika ligi kuu msimu huu,
wakati ligi daraja la kwanza lina timu kama Polisi Tabora, Polisi Mara,
Polisi Dar es Salaam, Polisi Dodoma.
" Hilo
linaanza msimu ujao. Hatuaziandikia barua timu Fulani tu, tumefanya
hivyo kwa vilabu vyote. Idadi ya timu haitapungua katika ligi kuu, ila
utafanyika utaratibu wa kutosha. Kwa mfano timu ambayo itabadilisha
umiliki itaendelea kubaki katika ligi. Kama bahati mbaya itatokea bahati
mbaya, timu ikafa, itaangaliwa namna ya kufanyika utaratibu mwingine.
Tunaamini kuwa kutoa kwetu taarifa mapema kutafanya kusiwepo na timu
yoyote itakayokufa.