Picha Ni Kwa Hisani Ya LindiYetu Blog |
Watu nane wamefariki dunia na tisa kujeruhiwa baada ya gari mali ya
mfuko wa hifadhi ya jamii TASAF wilaya ya Masasi kumkwepa mbuzi na
kuacha njia na kuua watu nane waliokuwa wamekaa pembezoni mwa barabara
kuu ya Lindi Mtwara.
Akizungumza na ITV kamanda wa polisi mkoa wa Lindi Tenatha Mzinga
amethibitisha kufariki kwa watu hao ambapo saba walikufa papo hapo na
mmoja amefariki asubui ya leo katika hospitali ya Nyangawa iliyopo jimbo
la mtama wilaya ya Lindi vijijini.
Akizungumzia mazingira ya ajali kamanda Mzinga amesema
imesababishwa na mwendo kasi wa dereva aliyefahamika kwa jina la Kesi
Mwaijande ambapo amesema baada ya kumwepa mbuzi alikosa mwelekeo na
kuwazoa.
Kwa upande wake daktari wa zamu Manfid Nyangali amethibitisha kupokea maiti zaba na majeruhi.
Wakizungumzia ajali hiyo wananchi wa kijiji cha Mtama jimbo la
Mtama wanahaya ya kusema gari hiyo yenye namba za usajili STl 1615
Landrover iliyokuwa imebeba madiwani sita wa halmashauri ya mji wa
Masasi ilikuwa ikitokea kwenye kilele cha maonyesho ya nanenane mkoani
Lindi.