Mimi mwenyewe imenishangaza hii mtu wangu kwamba watanzania
wameshauriwa kufuga na kula panya aina ya ndezi wakieleza kuwa nyama
hiyo haina mafuta mengi, ikiwa pia na virutubisho muhimu na vilivyo
adimu.
Hiyo ni kwa mujibu wa wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha
Sokoine (SUA) katika Maonyesho ya Vyuo Vikuu nchini yaliyofanyika jijini
Dar es Salaam hivi karibuni.
Wataalamu hao walisema kuwa ili kukabiliana na uharibifu wa kuchoma
moto misitu kwa ajili ya kuwatafuta wanyama hao, ni vyema wananchi
wakaanza kuwafuga kwa kuwa nyama yao ina ladha nzuri na ni laini.
Mhadhiri Mwandamizi wa SUA, Idara ya Uzalishaji, Mirende Matiko
alisema kuwa ingawa wanyama hao wanafugwa kwa wingi katika nchi za
Afrika Magharibi, hapa nchini ufugaji wake unakabiliwa na changamoto
nyingi.
“Wakulima wetu hapa tunawapa wafuge, siku chache baadaye ukienda
utaambiwa walikufa, lakini ukiwauliza majirani wanakuwambia ‘jamaa
aliwachinja’, ni sawa na kumpa mkulima mbegu halafu anakula,” alisema
Matiko.
Akizungumzia namna nyama hiyo inavyoliwa, Matiko alisema: “ Nyama
yake ina viinilishe vingi, yanatupwa manyoya na miguu yake tu, vitu
vingine vyote vinaliwa. Tena utumbo ndiyo mtamu sana, si unajua wanakula
nyasi tu.”
“Mtu akitaka kufuga wanyama hao anatakiwa kuwa na banda madhubuti
lenye ubora, chakula na maji safi yawepo bandani muda wote na
upandishaji ufanyike katika muda mwafaka,” alisema.
Mhadhiri huyo alitoa hadhari kwa wafugaji akiwataka kuwakamata
wanyama hao kwa umakini kutumia chandarua, kuepuka kusababisha majeraha.
Ndezi ni jamii ya nungunungu na pimbi, wakiwa wa aina mbili, ambapo
wadogo huwa na uzito wa kati ya kilo nne hadi sita na wakubwa hufikia
hadi kilo tisa. Wanyama hao hupendelea kuishi kwenye maeneo yanayolimwa
mashamba ya miwa, ulezi na mpunga.
Hata hivyo, Dk Loth Mulungu alisema kuwa wawindaji wa ndezi porini
husababisha madhara makubwa ikiwamo uchomaji wa misitu, uharibifu wa
bioanuwai, kukanyaga mazao mashambani na upotevu wa muda.
Mmoja wa watazamaji waliotembelea Banda la SUA, Elizabeth Maro
alisema kuwa ingawa kwa muda mrefu amesikia watu wakila mnyama huyo.
Binafsi hawezi kula nyama yake kwa kuwa anaamini hana tofauti na panya
wengine.
“Siwezi kumla kwa namna yoyote, huyu ni panya tu ndiyo maana hata
jina lake kwa Kiingereza anaitwa ‘canerat’, maana yake panya mla miwa


