![]() |
WATU binafsi na taasisi mbalimbali nchini
zimetakiwa kuendelea kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu,
ili kuwaendeleza na hatimaye waje kuwa na mchango kwa taifa.
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania
(TTCL), Amini Mbaga, alitoa wito huo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa
wiki alipokuwa akikabidhi msaada wa mifuko 70 ya saruji kwa ajili ya
kukisaidia kituo cha kituo cha Mama wa Huruma kuwa na majengo yake.
“Pamoja na kutoa huduma ya mawasiliano kwa jamii, pia huwa tunashiriki katika masuala ya kusajidia jamii,”alisema.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kituo hicho
kilichoanzishwa na watawa wa Kanisa Katoliki, Mtawa Berna Mdendemi,
alisema kituo kina watoto 70 ambao hawana wazazi, watoto wa mitaani na
wale wanaoishi mazingira magumu.
“Tuligundua kuwa watoto wengi katika maeneo haya walikuwa wanazagaa, hivyo tukaguswa na kuamua kuanzisha kituo hiki,”alisema.
Watoto hao wanasaidiwa kupata elimu ya awali, msingi, elimu ya stadi za maisha pamoja na malazi, chakula, na huduma za afya.
|

